CONTACT INFO
- PHYSICL ADDRESS:
- 16 Hatibu / 9th Road, Madukani Area
- PHONE:
- +255-(026)-2324661 / +255765530892
- EMAIL:
- info@biblesociety-tanzania.org
CUSTOMER SERVICE
- About Us
- Contact Us
- Bible Engagement
- Buy a Bible
- Membership
- Donate
Kiswahili ni lugha ya Taifa nchini Tanzania. Ni lugha yenye watumiaji wengi ukilinganisha na lugha nyingine zinazozungumzwa nchini. Historia inaonyesha, Tanzania ni nchi yenye makabila zaidi ya 125 yanayozungumza lugha tofauti tofauti. Kutokana na wingi wa makabila hayo,wapo watanzania hususani maeneo ya vijijini wasiojua Kiswahili na wanatumia lugha zao za asili katika kusoma na kuwasiliana. Chama cha Biblia kinalenga kuhakikisha kila mtanzania anafikiwa na Neno la Mungu kwa lugha yake na kwa bei anayoweza kuimudu. Katika Kuhakikisha hilo kuna miradi 10 ya tafsiri iliyoanzishwa, katika lugha ya Kikaguru, Kiha, Kihehe, Kirimi, Kinyiramba, Chasu, Kinyamwezi, Kifipa, Kinyia na Kirombo.
Tumefahulu kuwa na Biblia kamili 13 za lugha mbali mbali hapa nchini; Ambazo ni Kimochi, Kivunjo, Kimachame, Kidatooga, Kimasai, Kikurya, Kihaya, Kigogo, Kisukuma, Kiiraq, Kiswahili, Kinyakyusa na Kimachame.
Wananchi wengi Tanzania wanatumia lugha ya Kiswahili kama lugha ya mawasiliano nchini kote. Upatikanaji wa Biblia za Kiswahili katika mtandao utasaidia kuwafikia kwa urahisi na hivyo kuchangamana vizuri na Neno la Mungu.
Kutokana na kuongezeka kwa matumizi ya teknolojia, Wananchi wengi wameunganishwa na mtandao, hasa walioko makazini na wanafunzi wa vyuoni, hivyo wanaweza kupata maandiko kwa urahisi.
Nunua Biblia ya Kiswahili
Njoo, Tutafakari pamoja.
- Isaya 1:18
Mkutano Mkuu wa Wanachama 2022
-Unaweza kushiriki na sisi kwa kuwa na mwanachama wa Chama cha Biblia cha Tanzania na mwanachama wa Biblia kwenye klabu ya kuchangia kila mwezi
Tunashukuru kwa sala na msaada wenu juu ya kazi zetu za Chama. Ikiwa ungependa kujua zaidi kuhusu Vyama Vya Biblia ambayo hufanya miradi kwa wasemaji wa Kiswahili basi tafadhali bonyeza hapa:
https://www.unitedbiblesocieties.org/society/bible-society-of-tanzania
Unaweza pia kujua zaidi kwa kutembelea Mashirika haya ya Biblia:
http://biblesociety-kenya.org/
http://biblesociety-uganda.org/
http://biblesociety-rwanda.org/
15 Msiipende dunia, wala mambo yaliyomo katika dunia. Mtu akiipenda dunia, kumpenda Baba hakumo ndani yake. 16 Maana kila kilichomo duniani, yaani, tamaa ya mwili, na tamaa ya macho, na kiburi cha uzima, havitokani na Baba, bali vyatokana na dunia.
https://biblesociety-tanzania.org
https://shop.biblesociety-tanzania.org
Tel: +255-(026)-2324661
E-mail: info@biblesociety-tanzania.org
Click one of our contacts below to chat on WhatsApp
Social Chat is free, download and try it now here!